-->

Ray Kigosi Afungukia Unafiki wa Baadhi ya Mashabiki na Wapenzi wa Filamu

Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa baadhi wa Watanzania ni wanafiki na wamekuwa wakikatisha tamaa watu katika mambo yao kutokana na unafiki wao.

Ray Akiwa na Marehemu Kanumba (Maktaba)

Ray Kigosi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kusema kutokana na unafiki huo wa baadhi ya watu ulimfanya mpaka marehemu Kanumba kuvunjwa moyo katika kazi yake

Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, mara anatumia nguvu za giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza. Kanumba alipoenda ‘Big Brother’ alipondwa sana na kuitwa bogus kwa madai hajui kiingereza, ni watanzania hawa hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. Lakini leo wanamsifia hakuna kama Kanumba. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. Ila alisema maneno machache kuwa mtanikumbuka kama si leo basi ni kesho na alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba” alisema Ray Kigosi

Mbali na hilo Ray Kigosi amesema tasnia ya filamu si mtu bali ni mfumo, na si kuwa Kanumba na bongo movie kama ambavyo wengine wamekuwa wakidhani

Je, Kanumba kaondoka na bongo movie yake ya Freemanson? Kama wengine mnavyodhani Industry ni mtu sio system” alisema Ray Kigosi

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364