Ray Kigosi Atoboa Haya
Msanii wa filamu bongo Vicent Kigosi ‘Ray’, leo amekuja na mpya baada ya kusema yale aliyokuwa akiyafanya utotoni alipokuwa shule.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ray amesema alipokuwa mtoto alikuwa mtukutu na kukaa nyuma kabisa ya darasa kwa wale wanafunzi wanaojulikana maarufu kwa kupiga kelele, (backbencher) na kuwa wa kwanza kutoka nje kabla ya muda muafaka kufika.
Pamoja na hayo Ray amesema alipohitimu elimu ya sekondari alifeli na kupaa division four, lakini kitendo hiko hakikumkatisha tamaa na kufeli maisha.