-->

Riyama Afungukia Kukacha Shule!

RIYAMA Ally ameweka wazi kuwa hakumaliza elimu ya sekondari kutokana na ugumu wa masomo kwani hakuwa akiambulia chochote darasani licha ya walimu kujitahidi kufundisha kwa kiwango cha juu.

Mwanaspoti lilipiga stori na Riyama na alisema kutokana na kuona mambo magumu shule alilazimika kukatisha masomo yake na hivyo kuishia kidato cha pili.

“Kwa kweli ugumu wa masomo ulinifanya niache shule, niliona kama wazazi wanapoteza tu pesa yao bure, sikuwa naambulia chochote, walimu walikuwa wakijitahidi sana lakini sikuwa naelewa kitu, kwa hiyo nimekomea kidato cha pili, masomo magumu asikuambie mtu,” alisema Riyama.

Riyama ambaye amekuwa staa mkubwa kutokana na kuigiza filamu za ushari na zile za kusikitisha, amesema ameweza kumudu kuigiza katika vipengele mbalimbali vya filamu baada ya kubaini ana kipaji kikubwa na hana buni kukitumia vyema.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364