-->

Masogange Ashindwa Kujitetea, Hakimu Ampa Onyo

Kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili Video Queen, Agness Gerald ‘Masogange’ kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ambapo jana Alhamisi ilibidi aanze kujitetea baada ya kukutwa na kesi ya kujibu lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kile ilichodaiwa na mawakili wake kuwa walishindwa kumuandaa kutokana na kupatwa na msiba.

Agnes Masogange akiwa Mahakami (sio leo)

Masogange akiwa mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Wilbard Mashauri wakili anayemtetea Nehemia Nkoko alisimama na kumuomba hakimu hiyo awapangie siku nyingine ya kusikiliza kesi hiyo kwakuwa siku ambazo walipanga kumuandaa mshitakiwa huyo alipatwa na msiba hivyo isingekuwa vizuri kuanza kujitetea bila kumuandaa.

Baada ya Wakili huyo kutoa ombi hilo hakimu Mashauri aliwaambia jambo hilo lisitokee tena na kuwataka mawakili wa upande utetezi na mashitaka kupanga siku ambayo watakuwa tayari kuendelea na kesi hiyo.

Mawakili hao kwa kushirikiana na hakimu huyo walijadili kwa pamoja na kuafikiana kesi hiyo kurudi tena mahakamani hapo Januari 17 mwakani.

Baada ya kesi hiyo kuahirishwa Masongange alianza kujibanza ili kwenye kolido za mahakama hiyo ili kuwakwepa mapaparazi lakini nao walijibanza asiwaone ambapo alipojitokeza ili aondoke mapaparazi hao walimvamia na kuanza kumpigia picha mfululizo mpaka alipoingia ndani ya gari.

(Na Richard Bukos na Denis Mtima | Global Publishers)

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364