-->

Ray Kigosi na Johari Kuja na Tamthilia Mpya

Wasanii wa filamu wanaounda kampuni ya RJ Company, Brandina Chagula ‘Johari’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wanajiapanga kuingia kwenye biashara ya kuandaa tamthilia ambazo zitakuwa zinaonyeshwa katika runinga.

johari56

RJ Company ni miongoni mwa kampuni kongwe za filamu nchini ambazo mpaka sasa imeshaandaa filamu nyingi pamoja na kuibua vipaji vipya vya waigizaji.

Akizungumza katika kipindi cha Uhondo cha EFM, mmoja kati ya wakurugenzi hao, Johari Chagula, amezungumzia mipango mbalimbali ya kampuni hiyo.

“Kwa sasa bado tunaendelea kutoa filamu kama kawaida ila tunampango mkubwa zaidi, kuna tamthilia ya runinga ambayo inakuja, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Johari.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364