Akili the Brain Afunguka Kinacho Mkosesha Raha Kwenye ‘Game’
Msanii ambaye pia ni prodyuza Akili the Brain amesema anatamani apate mtu wa kufanya muziki anaoufanya wa Bongo Bangra, ili apate changamoto ya kuwa na mshindani.
Akili ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, na kusema kuwa anajisikia vibaya pale anapoona hakuna msanii mwengine anayefanya muziki huo.
“Kuna wakati nasikitika sana kwamba nakosa mtu wa kunipa changamoto za muziki niufanyao mimi, najua ntarudi vyema sana kwa kuwa mimi kiti changu hama mtu anayekalia, kwa sababu hamna mtu anayefanya muziki wa style yangu, napenda sana mtu ageze ili niwe na competitor fulani, lakini nikipata na wengine wanafanya muziki huu mi nitafurahi,” alisema Akili.
Pamoja na hayo Akili the Brain ametoa fursa kwa msanii ambaye atapenda kufanya aina ya muziki huo, amuone ili amfundishe iwapo atahitaji.
“Na kama hata haelewi itabidi aje kwangu mi nitamfundisha jinsi ya ku-flow na hizi style za Bongo Bangra”, alisema Akili.
eatv.tv