-->

Ray Kurudi na Nguvu Mpya Kwenye ‘Bongo Movie’

Msanii filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’ amefunguka na kuwaomba mashabiki zake kuwa tayari kuipokea kazi yake mpya ya ‘Gate Keeper’ ambayo ina utofauti mkubwa katika kazi zake alizowahi kuzifanya hapo awali.

Vincent Kigosi ‘Ray’

“Filamu yangu mpya itakuwa ya tofauti sana na itahusisha mastaa wengi kama Single Mtambalike ambaye amecheza kama Professa, Kajala Masanja aliyecheza kama mwananfunzi wa chuo kikuu, Baba Haji na wengine wengi na ninatarajia kuitoa tarehe 6 mwezi Machi”. Alisema Ray

Aidha Kigosi amesema kuwa upinzani kwenye filamu za ndani umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na wasanii wengi kuogopa kutoa filamu kutokana na uungwaji mkono mdogo wanaopata kutoka kwa mashabiki.

“Kipindi cha nyuma ilikuwa mtu akiongelea filamu Bongo basi anamuongelea Ray na marehemu Kanumba ila kwa sasa hakuna tena kwa kuwa watu wanaogopa kupeleka filamu kwa wasambazaji maana wanakosa kuungwa mkono na watu wa mitaani hivyo wanajikuta wanapata hasara badala ya faida kama kawaida”. Alisisitiza Ray

Msanii huyo amewaomba wananchi kuitafuta kazi yake hiyo mpya pindi itakapotoka ili waweze kujionea vitu vipya alivyokuja navyo.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364