Wema Sepetu Afunguka Anachokipenda Kwenye Siasa
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye wiki iliyopita amekihama chama chake cha muda CCM na kuingia CHADEMA amefunguka na kusema kuwa anaipenda sana siasa na siku akifanikiwa katika siasa atafurahi sana kwa kuwa ni kitu anachokipenda sana.
Wema Sepetu kupitia account yake ya Twitter amesema ameamua kuhama CCM na kuingia CHADEMA ili kupigania uhuru pamoja na demokrasia ambayo anahisi kwamba imeanza kupotea nchini Tanzania.
“Hicho ndicho tunachokwenda kupigania, uhuru tuliokuwa nao pamoja na democracy tunayoanza kuipoteza. God guide us. Hujajua tu ni jinsi gani siku nitakapofanikiwa kuwa mwanasiasa nitakavyo furahi… Naipenda siasa sana Maybe ni roots za Daddy” aliandika Wema Sepetu
Mbali na hilo Wema Sepetu anasema sasa hivi amekuwa na amani na furaha moyoni mwake.
” Saizi nina amani ya ajabu moyoni mwangu… I thank my Good Lord… Kweli kila kitu katika maisha hutokea kwa sababu, saizi niite kamanda ” alisisitiza Wema Sepetu
eatv.tv