-->

Richie: Msichana Anaweza Kubadili Jamii

MSANII mkongwe katika filamu Bongo, Single Mtambalike ‘Richie’ yupo mbioni kuachia kazi yake ya Queen of Maasai mwanzoni mwa Septemba ambayo anaonyesha jinsi gani msichana anaweza kubadili maisha ya jamii yake.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Rich alisema waigizaji wengi wanakimbilia kutengeneza filamu za kimapenzi, lakini yeye kama mkongwe, ameamua kuonyesha jinsi msichana mdogo anavyoweza kubadili maisha ya jamii yake kama akipata fursa na kujielewa.

“Hii ni filamu iliyochezwa umasaini, inaonyesha jinsi msichana wa kimasai anavyoweza kubadili maisha ya jamii yake. Tumezoea wamasai ni wafu-gaji, wasi-ojali elimu, lakini katika filamu hii inaonyesha mageuzi katika jamii yanaweza kufanywa na msichana, tofauti na fikra za wengi kuwa wanaume ndiyo wa kubadili mambo,” alisema Rich ambaye ni mmoja wa waigizaji mahiri nchini.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364