-->

Roma Mkatoliki Aibukia Kenya

Rapa Roma Mkatoliki ambaye amerudi na ujio wa nguvu na ngoma zake ‘Zimbabwe’ na ‘Hivi ama vile’  baada ya kukaa kimya muda mrefu baada ya kupata matatizo ya kutekwa sasa ameibukia nchini Kenya.

Roma Mkatoliki pamoja na Stamina

Roma Mkatoliki pamoja na Stamina ambao kwa pamoja wanaunda umoja wao unaofahamika kwa jina la ‘Rostam’ wameanza kupiga hatua mbele zaidi ya kutangaza muziki wao na kuwafikia mashabiki nje ya Tanzania baada ya wakali hao kuonekana nchini Kenya wakifanya ‘Media tour’

Umoja wa Roma Mkatoliki na Stamina unafahamika zaidi pindi wakali hao wanapokutana kwenye jukwaa moja na kutoa burudani kwa mashabiki kwani kwa uwezo wao huwa wanaweza kuamsha mashabiki na kutoa burudani ya nguvu.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364