-->

Ujumbe mzito wa Shamsa Ford kwa Chidi Mapenzi

Mrembo kutoka kiwanda cha filamu Bongo,  Shamsa Ford  ametimiza mwaka mmoja wa ndoa yake na mumewe mfanyabiashara Rashidi Saidi maarufu kama Chidi Mapenzi.

Katika kusherekea mwaka  mmoja huo , Shamsa amempa  mzito mumuwe kuhusu  ndoa yao, yenye mwaka mmoja.

“Leo tumetimiza mwaka mmoja wa ndoa yetu.Tumepitia changamoto nyingi sana kwa muda mfupi wa ndoa yetu ila hatujawahi kuchokana kwasababu Mwenyezi Mungu ndo alituunganisha. Upendo wako kwangu unanifanya nijione mwanamke mwenye bahati duniani na inatosha..Mwenyezi Mungu azidi kutupigania kwenye hii safari ndefu tuliyoianza. Nakupenda, na nakuheshimu sana mume wangu RASHIDI..HAPPY ANNIVERSARY TO US,” ameandika Shamsa katika mtandao wa Instagram.

Shamsa aliolewa mwaka jana Septemba 2, ndoa hiyo iliudhuriwa na watu wa karibu wa mrembo huyo na wa mumewe. Kwa mwaka mmoja wa ndoa ya wawili hao bado hawajabahatika kupata mtoto.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364