-->

Roma Mkatoliki: Babu Tale Alinichimba Mkwara

Msanii Roma Mkatoliki ambaye leo ameachia ngoma yake mpya ‘Kaa tayari’ amefunguka na kusema moja ya mstari uliopo kwenye wimbo wake huo unamuhusu meneja wa Diamond Platnumz ambapo unamchana kuwa saizi anamganda sana Diamond Platnumz mpka amelisahau kundi lake na Tip Top Connection.

ROMA 34

Roma Mkatoliki amedai kabla ya wimbo huo haujatoka aliweza kusimkilizisha Babu Tale kisha Bab Tale alimchimba mkwara kuwa usipofuta huo mstari wimbo wako hautatoka, Roma aliongea huku akiwa anacheka kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio.

Kwa upande wake Babu Tale aliibuka kwenye kipindi hicho na kuja kujibu tuhuma hizo na kusema yeye hajalisahau kundi hilo kama ambavyo Roma Mkatoliki alivyoimba bali anadai wao wana mipango, ndiyo maana alianza kuja Madee na Miguru pande, akaja Dogo Janja na ‘My Life’ na baadaye atakuja Tunda Man, hivyo hajalisahau kundi hilo kama alivyosema Roma Mkatoliki kwenye wimbo wake huo.

“Unajua saizi Babu Tale ni meneja mkubwa Afrika, nimemzidi Roma Mkatoliki kwa kila kitu, nimemzidi followers, busara, hadi dhambi nimemzidi, hivyo Roma Mkatolik mimi nadhani ameimba huo mstari kwa kuwa anajua mimi ni mtu mkubwa hivyo alikuwa anataka wimbo wake uweze kufanya vizuri ndiyo maana akanichana mle, japo alichoimba hakina ukweli” alisema Babu Tale.

Kwa upande wa Said Fella alisimama upande wa Roma Mkatoliki na kudai alichoimba Roma Mkatoliki ni maneno ambayo hata mtaani yapo kwani watu wamekuwa wakisema kuwa viongozi hao saizi wameyasahau makundi yao ya zamani.

“Unajua Roma ni mtu mzima, alichoimba hata mtaani huko watu wanasema, na unaweza kuona labda Roma ameambiwa hayo maneno na msanii kama Madee au msanii mwingine yeyote wa kwetu, lakini hata mimi nilishawahi kumwambia mdogo wangu Babu Tale kuwa tufanye yote lakini yeye asiisahau Tip Top Connection na mimi nisiisahau TMK” alisema Said Fella.

eatv.tv

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364