-->

Tetesi:Masogange, Rammy Galis Wamwagana

Kimenuka! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia ubuyu ulioenea ‘town’ kuwa uchumba wa mastaa wapenzi Bongo, Rammy Galis na Agness Gerald ‘Masogange’ unadaiwa kuvunjika.

Agnes masogange na rammy

Ubuyu huo ulianza kutapakaa baada ya picha ya Rammy ambaye ni mwigizaji wa Bongo Muvi na Masogange kuwekwa kwenye kurasa mbalimbali za Mtandao wa Kijamii wa Instagram huku zikiwa zimeambatana na maneno yanayodaiwa kuandikwa na jamaa huyo.

Maneno hayo yalisomeka: “Kwa nini mtu husahau wema wote uliotenda? Utu wako wote unakosa thamani kwa kosa moja ulilotenda, machozi humtoka mwanadamu pindi maumivu yakizidi moyoni.

“Unalia na kukesha kuomba msamaha lakini mwenzio bado na ndiyo kwanza kamuweka mwanaume mwenzako kwenye WhatsApp yake, sitakuja kusahau kwenye maisha yangu, nimeumizwa, leo nakubali.”

Picha hiyo ilipotupiwa mtandaoni, watu mbalimbali walianza kushusha ‘komenti’ huku wengine wakimchana mshikaji huyo kuwa u-handsome si kitu mjini bali mkwanja ndiyo kila kitu na kama angekuwa vizuri, asingekimbiwa na mwanadada huyo.

WIKIENDA HALIKO NYUMA

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Wikienda halikuwa nyuma, liliingia mzigoni na ‘kukontakti’ moja kwa moja na Rammy ili kusikia yaliyomo yamo? Alipopatikana alisomewa kilichokuwa kinaendelea mtandaoni ambapo alishikwa na kigugumizi huku akidai hataki kulizungumzia jambo hilo hivyo liachwe kama linavyoonekana mitandaoni.

“Hili suala siwezi kabisa kulizungumzia, ninyi liacheni hivyohivyo maana hata kama nimeachwa sidhani kama inawahusu ni mambo binafsi na mimi ningependa tuongelee kazi kwa sasa basi,” alisema Rammy.

RAMMY ABANWA

Mwanahabari wetu aliendelea kumbana Rammy ili kupata ‘floo’ yake ilivyokuwa kama ifuatavyo…

Wikienda: Rammy, pamoja na kuwa umelizungumzia kwa kifupi, funguka ili mashabiki wako wajue kinachoendelea kati yako na Masogange.

Rammy: Unajua sababu ya kutoongea haya mambo ya Masogange ni kwa sababu nina mpenzi wangu ambaye tuko sawa, nikiendelea kumpaisha huyo nampa kiki bure, huenda mambo yakaniharibikia.

Wikienda: Hata hivyo, bado hujafunguka vizuri kwani ishu ni nini kimetokea hadi mkazinguana, maana floo ya ujumbe mtandaoni inaonesha wewe ndiye chanzo cha kumwagana kwenu?

Rammy: Nimeshakwambia haya mambo sipendi kuyapa nafasi tena kama imeshatokea, imetokea, ukinihitaji nitafute kwa masuala ya kazi tu!

MASOGANGE ASAKWA

Baada ya kumsikia Rammy, Wikienda lilimwendea hewani Masogange ambaye ni video queen Bongo na kumsomea mashtaka yake lakini alipopokea alisikiliza kisha akakata simu, alipopigiwa tena hakupokea na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu pamoja na kwamba ulionesha umepokelewa kwake.

WALIKOTOKA

Uhusiano wa wawili hao una miezi kadhaa tu ambapo kabla ya kuibuka kwa figisufigisu wamekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwani baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiifurahia ‘kapo’ yao hivyo ubuyu wa kumwagana kwao utaibua mjadala mpya.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364