Uwoya: Nikilala, Nikiamka Nawaza Siasa Tu
STAA mkali Bongo Muvi, Irene Uwoya amefunguka kuwa bado hajakata tamaa ya kuwa mwanasiasa japokuwa mwaka jana alishindwa lakini hiyo imempa nguvu ya kujipanga zaidi na kwamba kwa sasa akili yake yote akilala, akiamka ni kuwaza siasa tu.
Akizungumza na Amani Uwoya alisema kuwa, changamoto alizozipitia kipindi cha kampeni zimemfundisha mambo mengi na pia zimemkomaza na kufanya damu yake izidi kupenda siasa.
“Bado siasa ipo kwenye damu na nimepata changamoto kubwa sana kipindi kile cha nyuma na sasa nipo tayari kuingia vitani tena ili niweze kuongoza wananchi wangu na nifanye kila ambacho wamekikosa kwa muda mrefu,” alisema Uwoya.
Uwoya alikuwa akigombea Ubunge wa Viti Maalum Tabora, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini alishindwa kwenye ngazi ya Taifa.
Chanzo:GPL