Rose Ndauka Azindua Lebo Ya ‘Ndauka Music’
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka, kupitia kampuni yake ya Ndauka Adverts Ltd, leo amezindua lebo ya muziki iitwayo Ndauka Music ambayo itatoa fursa kwa wanamuziki nchini, hususan wanaochipukia, ili kujitangaza.
Uzinduzi huo ulifanyika ofisini kwake Sinza, jijini Dar es Salaam, maeneo ya Sinza-Afrika Sana karibu na ofisi za Mamlaka ya Kodi (TRA) Mwenge, ambapo alimtangaza msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Casso ambaye leo ameachia rasmi video ya ngoma yake iitwayo ‘Kitonga’.
Akizungumzz na waandishi wa habari, Rose alisema ameichunguza sekta ya muziki kwa kipindi kirefu pamoja na kumpika msanii huyo kwa muda usiopungua mwaka mmoja hadi kuamua kumtoa hivyo ana ujuzi na kile anachokifanya.
“Wengi wamenizoea kwenye filamu, lakini mbali na hilo mimi ni shabiki mkubwa wa muziki kwa hiyo naelewa kila kitu kuhusu hii fani, nimeamua nianze na huyu kwanza kisha wengine watafuata. Wapo kama watatu kwenye lebo yangu lakini sitaki kuwatoa wote kwa mkupuo,” alisema.
Chanzo:GPL