-->

Z Anto:Nawakubali sana Alikiba na Dully Skyes

Msanii Z Anto ambaye kwa sasa yupo katika mchakato wa kutaka kurudi kwenye muziki wa Bongo Fleva amefunguka na kusema kuwa katika wasanii wa Bongo Fleva anaowakubali na kuwaheshimu ni Alikiba pamoja na Dully Skyes.

z-anto

Z Anto alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio ambayo kwa jana ilikuwa ikiruka moja kwa moja kutokea Kigamboni Dar es Salaam, Z Anto amesema wasanii hao kwanza wanajivunia sauti zao nzuri lakini pia wote kwa pamoja wana uwezo wa kufanya muziki wa aina yoyote na kwa muda wowote na wakafanya vyema.

“Mimi nawakubali sana Alikiba pamoja na Dully Skyes, Dully Skyes kwanza anaweza kuimba, akafanya dance hall, reggae, na anaweza kupotea kwenye muziki kwa miaka na akarudi akashika nafasi yake ile ile, hivyo hivyo kwa Alikiba. Lakini pia Alikiba ana sauti ya kipekee sana sauti yako ina ‘Auto tune’ ya asili ambayo huwezi kuipata kwa wasanii wengine, lakini pia na yeye anaweza kupotea miaka mitatu na akirudi anashika nafasi yake” alisema Z Anto

Mbali na hilo Z Anto alisema kuwa muziki wa Bongo Fleva saizi ni mwepesi sana kulinganisha na wakati wao wanatoka na kusema hiyo haimpi ugumu yeye kurudi sababu muziki wa sasa ni mwepesi hivyo ana uhakika akirudi atafanya vyema.

“Muziki wa sasa umekuwa mwepesi sana, watu wanaimba imba tu wanatoka, muziki huu ukiwa na ‘Six Packs’ ukiimba unatoka si muziki wakunipa changamoto mimi” alisema Z Anto

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364