-->

Rose Ndauka Hajali Nyumba Yao Kuvunjwa

WAKATI mamia ya wakazi wa Dar es Salaam waishio mabondeni na pembezoni mwa bahari na mito wakihaha nyumba zao kuvunjwa, staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema hajali kama nyumba yao itakutwa na bomoabomoa hiyo.

ROSE NDAUKA345

Badala yake, alimpongeza Rais John Magufuli kwa kusimamia zoezi hilo, kwani wengi wa wanaobomolewa walishapewa taarifa mapema na hawakutii agizo hilo la serikali, lakini akaitaka kuwaangalia kwa jicho la tatu watu ambao hawakupewa taarifa za zoezi hilo.

“Wazazi wangu wakibomolewa nyumba naona kawaida tu, siwezi kuwa na presha maana kila kitu kinapangwa na Mungu, kama ni kubomoa wabomoe tu hatuna la kufanya,” alisema Rose.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364