Ruby Sina Ukaribu na Ali Kiba
BAADA ya habari kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikihoji ukaribu unaohusishwa na kutoka kimapenzi baina ya waimbaji nyota wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ na Ali Kiba, mrembo huyo amesema hana ukaribu wowote na msanii huyo.
Ruby anayefanya poa na ngoma yake ‘Walewale’ amelipasha Swaggaz kuwa taarifa za ukaribu wake na Kiba amekuwa akiziona kwenye mitandao ya kijamii lakini hakuna kinachoendelea kati yao kwani hata namba yake ya simu hajawahi kuwa nayo.
“Na mimi taarifa hizo nimekuwa nikiziona kama wewe ulivyoziona, sioni jipya kwasababu walishawahi kusema kuwa nipo karibu sana na Diamond, sasa wamegeukia kwa Kiba ambaye hata mawasiliano yake sijawahi kuwa nayo,” alisema Ruby.