-->

Saguda: Sijaona Mwanamke wa Kumfananisha na Recho

Ni mwaka wa pili sasa tangu mwigizaji wa filamu za Kibongo, Recho Haule ‘Recho’ kufariki dunia, mume wake Saguda amesema mpaka sasa hajaona mwanamke wa kufanana naye.

Saguda

‘’Kiukweli ndani ya miaka hii miwili sijaona mwanamke wa kumfananisha tabia na Recho alikuwa na tabia za kipekee sana  na upendo wa dhati’’ Alisema Saguda.

‘’Kitu ambacho ni deni kwangu kwa mke wangu marehemu Recho nilitaka mke wangu aishi maisha ambayoitakuwa funzo kwa watu, mimi na Recho tulitoka kwenye dhiki na alipigwa vita na marafiki hadi ndugu zake walimwambia kwanini anaishi na mimi lakini aliwaambia ananipenda hata kama sina kitu, tulitoka kwenye ‘zero’ hadi tukafungua kampuni hadi anafariki tulikuwa tumetoa filamu ya pili’’ alisema Saguda

‘’ Kiukweli huwa sipendi kuonana na rafiki yake Recho aitwaye Odama kwasababu walikuwa marafiki sana kwahiyo nikimuona huwa nakumbuka mbali sana naona bora nimkwepe’’Aliongeza Saguda.

‘’Leo kutakuwa na misa pale Kinondoni, Makaburini kuanzia saa tisa kamili nawaomba watu wote wajitokeze kwa wingi,Alisema Saguda.

rachel1

Recho Enzi za Uhai wake

Cloudsfm

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364