Hakuna wa kufanana na Ngwea bongo – TID
Msanii TID amesema mpaka sasa kwenye maisha yake ya muziki hajawahi kuona msanii ambaye atachukua kiti cha aliyekuwa mkali wa ‘free style’ bongo, Albert Mangwea, aliyefariki miaka mitatu iliyopita.
Akijibu swali la mtangazaji wa kipindi cha Friday Night Live Sam Misago, alipomuuliza iwapo kuna msanii yeyote anayefikia uwezo wa Ngwea, TID alisema mpaka sasa hakuna wa kuweza kumfananisha na Ngwea.
‘What are u saying…! Ngwea!? Hakuna msanii anayeweza kumfikia Ngwea, that man was special, Ngwea alikuwa blessed! Alafu umfananishe na nani…Bill Nas anaweza kuwa a half of it lakini hawezi kuwa kama Ngwea, Ngwea can rap, Ngwea can sing, Ngwea can give u a melody..alafu umfananishe na mtu, hakuna wa kufanana naye, no one!”, alisikika TID akijibu.
Pamoja na hayo TID amesema yeye kama rafiki yake ataendelea kuenzi kazi zake, na amewashukuru wasanii waliojitokeza kufanya show ya kumbukumbu yake, na kuweza kumsaidia mama mzazi wa Albert Mangwea ikiwa kama kumuonyesha kuwa walikuwa wanampenda mtoto wake.
eatv.tv