-->

Saida Karoli: Kuhusu Wimbo wa Salome, Siujui Mkataba na Diamond, Wala Sijawahi Kuonana Naye

BAADA ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kuachia ngoma ya Salome ambayo ndani yake ametumia melodies na vionjo vilivyomo kwenye wimbo wa mwanadada aliyetamba na kujichukulia heshima kubwa kwenye muziki wa asili hapa nchini, Saida Karoli, taarifa zilianza kuzagaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa Mbongo Fleva huyo ameiba wimbo wa Saida bila makubaliano rasmi.

Kufuatia tuhuma hizo, Diamond aliamua kufunguka na kukanusha taarifa hizo huku akieleza namna walivyokubaliana na uongozi wa Saida kupitia meneja wake ambaye ni Felician Mutta kabla ya kuiachia ngoma hiyo kuwa atalipa asilimia 25 ya publishing ambayo itaenda kwa Saida.

Mwenye Wimbo wake kaja

Kutokana na maelezo hayo, Saida Karoli ameamua kuanika yote ya moyoni na kueleza kuwa hajawahi kufunga mkataba na Diamond kuhusu wimbo wa Salome wala hajawahi kukutana naye.

“Mimi nimefurahi Diamond kurudia wimbo wangu wa Salome, inaonesha jinsi kazi zetu zinavyothaminiwa pamoja na kuukuza utamaduni wetu…..”

“Hiyo asilimia 25 na mimi nimezisikia tu wakati Diamond akihojiwa, labda atakuwa amempatia Meneja wangu Felician Mutta, kama ingelikuwa inakuja mfukoni mwangu ningelijua ni shilingi ngapi…”

Kuhusu Mkataba?

“Huu mkataba unaoongelewa (mkataba na Diamond kuhusu kutumia wimbo wa Salome) mimi siujui  na sikuuona wala hakunijulisha kama kuna mkataba…. Bali aliniambia Diamond anataka kuutumia wimbo wako, ila siyo kibiashara na mimi nikamruhusu na hata baadaye niliposikia kwamba kuna mkataba kuhusu huo wimbo sikuona sababu ya kumuuliza meneja wangu wala kufuatilia, niliona nitapata vingi na vingi na vingi.”

Tangu wimbo wa Salome utoke amewahi kuonana na Diamond ana kwa ana?

Sijawahi kuonana naye, ila tuliongea kwenye simu tena simu siyo ya Diamond ilikuwa ni ya Meneja wangu huyo wa zamani, Felician Mutta.”

Kumbe hana Mkataba na meneja wake Felician Mutta, hali iliyopelekea akaanza kuomba omba.

“Mkataba wangu na Felician Mutta uliisha mwaka 2007, ndipo nikaanza kujidhatiti mimi kama mimi, nikaanza kuomba misaada sehemu mbalimbali kutumia vyombo vya habari….. Tivoli Studio naye mkataba ulikwisha lakini walinisaidia, walinipa kiwanja Mwanza nikajenga nyumba ndiko ninakoishi na familia yangu.”

“Niliomba misaada kwa kuwa nilichokuwa nakipata kilikuwa hakitoshi kwa wakati huo, maana menejimenti inataka pesa na msanii pia, na mameneja wa Tanzania siyo sawa na mameneja wa Ulaya.”

Kuhusu kufanya kazi na Diamond

“Napenda kazi zake, na ndiyo maana sijataka anilipe hata mia, na hata kama akitaka kutengeneza wimbo na mimi nitanfa hata kama ni mpya, bila hata kunilipa.”

Kuhusu kulipwa ile asilimia 25?

“Mimi ndiye mwenye wimbo, nimemruhusu Diamond atumie huo wimbo na hata asipolipa hizo asilimia 25 hakuna atakayemshtaki. Na kama asilimia 25 (pesa walizokubaliana na Meneja Mutta) hazijanifikia, inamaana Diamond ametapeliwa.” Alimaliza kwa kusema hivyo Saida Karoli.

Hapa chini nimekuwekea full video ya mahojiano hayo, itazame na uisikilize kwa makini mwanadada Saida akifunguka.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364