-->

Chuchu Afungukia Kuficha Ujauzito Wake

Msanii wa filamu za bongo Chuchu Hansy amezungumzia sababu ya ujauzito wake na kusema kuwa hajataka kuweka hadharani kwani ni kitu binafsi.

Chuchu Hansy – Msanii wa filamu

 

Akizungumza na East Africa Television, Chuchu Hansy amesema taarifa za yeye kuwa na ujauzito ameamua kufanya siri kwani anaona si vyema kuzungumzia vitu binafsi hadharani hususani kwenye mitandao, na kwamba muda muafaka ukifika kila mmoja atajua ukweli.

“Unajua vitu kama hivyo ni too personal na nisingependa kuviongelea especialy kwenye media, lakini muda muafaka ukifika kila mmoja atajua nini ni nini, ila kwa sasa acha ikae hivyo watu waendelee kuhisi”, alisema Chuchu.

Chuchu ambaye ameibuka mshindi katika kipengele cha muigizaji bora wa kike kwenye EATV AWARDS, amekuwa gumzo mtandaoni kwa kuficha taarifa za ujauzito wake, tofauti na wasanii wengi wa kike wanavyofanya siku hizi.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364