Serikali Hii ya Dk Magufuli Tutafanikiwa -Dk Cheni
Msanii wa filamu nchini Dkt Cheni amesema ana imani kubwa sana na serikali ya Rais Dkt John Magufuli kwamba itawasaidia wasanii katika kuondoa tatizo sugu la kuibiwa kwa kazi zao na kuuzwa kwa bei ya chini.
Cheni ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku jumatatu hadi ijumaa.
”Tumekuwa hatufaidiki kwa kazi zetu tunazozifanya ila kwa serikali hii ya Magufuli na ufanisi wake hapa hakuna shaka tutafikia melengo vizuri, mwenyewe nina ‘movie’ ambazo zipo tayari zaidi ya 10 nangojea tuu mambo yawekwe sawa niziachie”.-Amesema Dkt Cheni.
Aidha Dkt Cheni amebainisha kuwa wanatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wao hivi karibuni kama walivyokubaliana na waziri Nape Nnauye ili waweze kushughulikia kikamilifu vikwazo vyote vinavyowafanya kushindwa kufikia malengo wanayokusudia.