-->

Shamsa Ford Apigia Saluti Wabongo wa Instagram

Msanii wa filamu bongo, Shamsa Ford amefunguka mapya kwa kudai laiti watu wangekuwa wanaitumia vizuri mitandao ya kijamii basi wangekuwa wamefika mbali kimaendeleo lakini wamebakia katika kutengenezea mambo ya uongo tu.

Shamsa amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kukerwa muda mrefu na watu wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii kuanzisha mijadala ambayo haina ukweli wowote wala kuwa na taswira nzuri katika jamii.

“Nina imani hii mitandao tungeitumia vizuri tungekuwa na maendeleo makubwa,ila unavyotumika jamani ni kero. Sisi wabongo ni kiboko aise, wabongo wa instagram ni kiboko Wallah, mtu anaweza akatengeneza jambo likafanana na ukweli mpaka mwenyewe ukachoka. Wabongo tuna vipaji”¬†aliandika Shamsa.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364