-->

Sitegemei Mwanaume Kufanya Kazi Zangu- Aisha

AISHA Bui mwigizaji wa filamu wa kike amefunguka kwa kusema kuwa yeye katika kuandaa kazi zake za filamu hakuna mchango wowote anaotegemea kutoka kwa mwanaume bali ni kazi ya jasho lake hawezi kuandaa sinema yake na kusubiri hela kutoka kwa Pedeje.

“Kazi ya utengenezaji wa filamu kwangu naichulia kama sawa na biashara nyingine, hivyo ninavyotengeneza na kutumia pesa yangu si kutoka kwa mwanaume kama wengine wapo hivyo mimi ni tofauti,”alisema Aisha.

Mwigizaji huyo anasema kuwa anapowekeza fedha katika sinema lengo lake kubwa ni kuweza kuzungusha mtaji wake endapo atakuwa akitegemea pesa kutoka mwanaume hawezi kufikia malengo kwani muda wote atataka kumwangalia mwanaume na y eye hataki kuwa tegemezi, ndio maana akatafuta mtaji wake.

Msanii huyo anasema kuwa unapoingia katika kazi yoyote lazima ujipange kwa ajili ya kulinda mtaji wako na kuuendeleza kwa ajili ya kuepukana na utegemezi wa pesa kutoka kwa wanaume wakati wana nguvu na uwezo wa kujitafutia kipato chao.

FilamuCentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364