-->

Shamsa Ford Atoa Ushauri Huu kwa Vijana

Muigizaji wa filamu nchini Shamsa Ford ametoa ushauri kwa Watanzania hususani vijana ambao hupata kidogo na kushindwa kujipanga na maisha ya kile kidogo wakipatacho na kusema siku zote unapaswa kuthamini kile ulichonacho leo ili kuwa na kesho nzuri.

Shamsa Ford ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa ujumbe huo kwa vijana na kuwaasa kutodharau kabisaa kidogo wakipatacho kwani hicho ndicho kinaweza kufanya watu wapige hatua.

“Binadamu wa kawaida hupenda kuweka umakini mkubwa kwa kile asichonacho badala ya kile alichonacho. Analaumu kwa sababu ya asichonacho badala ya kushukuru kwa sababu ya alichonacho. Wengi hufikiri sana kuhusu kesho na kuacha kutumia leo waliyonayo. Wanapoteza muda wa sasa wakitarajia kuwa kesho ipo. Ukiona unadharau ‘kidogo’ ulichonacho kwa sababu ya kile ‘kikubwa’ unachotarajia, jua upo katika mchezo wa kufukuza upepo. Leo ni mbegu ya kesho unayoitarajia. Ulichonacho ndicho kimebeba mimba ya unachokitarajia. Usipokuwa mwaminifu kwa ulichonacho, sahau kuhusu unachotarajia” aliandika Shamsa Ford.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364