-->

Shamsa Ford Atoa Wito kwa Wanawake Kupinga Tabia Hii ya Baadhi ya Wanaume

Shamsa Ford

Shamsa Ford

Shamsa Ford kutoka kiwanda cha filamu Bongo amezungumza kwa mara nyingine tena sababu ya kuachana na aliyekuwa mzazi mwenzie, aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume kuwa ni Vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mzazi mwenzie huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shemsa Ford ameandika hivi:

Wanawake wenzangu tusimame kwa pamoja na tukemee hii tabia ya kupigwa na wanaume. .si mbaya ni kijitolea mfano mimi ili kuwapa moyo wanawake wenzangu. .Nakumbuka wakati nina mimba ya Terry ya miezi 5 nilipigwa mitama na kipondo cha hali ya juu mpaka nikapoteza fahamu.Nilipelekwa hosptal kwa bahati nzuri mtoto wangu hakudhulika..maisha ya kipondo yaliendelea na kwakuwa nilimpenda sana yule mwanaume nilivumilia na kuhisi labda atabadilika. Lakini hakuweza kubadilika na mwisho wa siku nikaamua kuchukua maamuzi magumu ya kuachana naye. Namshukuru Mungu nina maisha ya furaha na amani kabisaa na mwanangu. …WEWE mwanamke unayevumilia hivi vipigo jua wewe ni kiumbe muhimu na unathamani katika hii dunia. ..#KEMEA KIPIGO#

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364