Shamsa Ford Kufunga Ndoa Ijumaa Hii
Msanii wa filamu Shamsa Ford anatarajia kufunga ndoa Ijumaa hii na mfanyabiashara wa nguo aitwae ‘Chidi Mapenzi’.
Muigizaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa ndoa hiyo itafanyika nyumbani kwa wazazi wake Sinza Africana jijini Dar es Salaam.
“Kweli bhana Ijumaa hii Mungu akipenda nafunga ndoa,” alisema Shamsa Ford.
Miezi mitatu iliyopita mfanyabiashara huyo alikiri kuwa kwenye mahusiano na malkia huyo wa filamu na kuweka wazi mpango ya ndoa.
Bongo5