Shamsa Ford Kuzaa ‘Kijiji’
WAKATI watu wa kada mbali-mbali wakielezea uwepo wa hali ngumu ya kiuchumi nchini, Muigizaji Shamsa Ford ambaye miezi michache iliyopita aliolewa, amesema anataka kuzaa watoto wengi (kijiji) wapatao saba, tena kwa haraka haraka.
Akizoza na mwanahabari wetu, Shamsa alisema hivi sasa yupo katika harakati za kuusaka ujauzito kwa hali na mali, kwani licha ya mambo kuwa magumu kiuchumi, anaamini kila mtoto huzaliwa na riziki yake, hivyo hajali kuhusu malezi.
“Kila mtoto anakuja na riziki yake kwa hiyo nitazaa tu, vile tuko wawili na baba yao tutawalea vizuri tu maana tunafanya kazi, nimeshaanza kutafuta ujauzito tayari na ninamuomba Mungu anisaidie niweze kutimiza hilo lengo maana hata katika familia yetu tumezaliwa saba,” alisema Shamsa.
Chanzo:GPL