-->

Shamsa: Siwezi Kumhukumu Nay

STAA wa Bongo Muvi, Shamsa Ford kwa mara ya kwanza ameibuka na kuiongelea Ngoma ya Shika Adabu Yako iliyoimbwa na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwa kamwe hawezi kumhukumu Nay kwa maneno aliyoimba.

SHAMSA21

Akigonga mbili-tatu na Showbiz, Shamsa aliyewahi kubamba na Filamu ya Chausiku alisema kuwa aliusikia wimbo huo uliowachana mastaa wengi wa Bongo Muvi na kwamba bado hajajua kinachomfaidisha Nay kupitia wimbo huo.

“Namuacha kama alivyo na kamwe siwezi kumhukumu kwa kile alichokiimba labda kwa upande wake aliona ni sawa,” alisema Shamsa.

Katika Wimbo wa Shika Adabu Yako, Nay amewachana mastaa wa Muziki na Bongo Muvi ambao ni Shetta, Ommy Dimpoz, Ray, Niva, Wema Sepetu na wengine wengi jambo lililosababisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi na kudhalilisha watu.

Chanzo: GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364