-->

Shamsa Yupo Tayari Kuachika!

STAA wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford ambaye ni mke wa ndoa wa mfanyabiashara Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ amefunguka kuwa, yupo tayari kupewa talaka kuliko kuacha kazi yake ya uigizaji.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shamsa alisema kuwa, ikitokea mumewe kumtaka aachane na uigizaji atamuomba talaka kwani hayupo tayari kuachana na kazi hiyo kwa sababu anaipenda na ndiyo iliyomtoa kimaisha.

“Hata nikiambiwa nafunguliwa biashara ya mabilioni au nipewe hizo fedha ili niache kuigiza sitakuwa tayari kwa kweli, niko tayari kupewa talaka lakini siyo kuacha filamu japokuwa kwa sasa soko limeshuka lakini nitaendelea kuigiza mpaka mwisho wa maisha yangu,” alisema Shamsa.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364