-->

Sijampiga Dongo Wolper Aku Raha ya Serengeti Naijua Mimi- Nisha

”Salma Jabu” Nisha muiogizaji wa filamu swahilihood.[/caption]NYOTA wa filamu Bongo Salma Jabu ‘Nisha’ amesikitishwa na baadhi ya watu ambao wanajaribu kumtengenezea ugomvi na msanii mwezake wa kike Jack Wolper kwa kutafsiri ujumbe wake alioposti katika ukurasa wake kama ilikuwa ni dongo akimpiga msanii mwezake.

“Jamani sipendi kinachoendelea mimi siwezi kumuingilia Wolper awe na nani, na asiwe na naye, kingine raha ya Serengeti naijua mimi sasa hivi nimestaafu tu na kuiacha mbuga mapenzi yana siri nzito,”alisema Nisha.

Nisha alisisitiza kuwa yeye hakumpiga mtu dongo bali ana haki na uhuru wa kuposti chochote katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii kama wafanyavyo wengine, kwani kufanya hivyo kunaweza kujenga chuki kati yao bila ukweli wowote bali ni tafsiri tu ya watu.

Filamucentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364