-->

Shilole Adaiwa Kumlewesha Dogo

Baada ya msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, hivi karibuni Ijumaa lilinyetishiwa kuwa, amejiweka kwa dogo mmoja aliyefahamika kwa jina la Medy Music ambaye wamekuwa wakipika na kupakua kwenye nyumba ya staa huyo iliyopo Kijitonyama jijini Dar.

SHILOLEQ2

Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu juzikati jioni alitinga nyumbani kwa Shilole na kufanikiwa kuwakuta wawili hao lakini katika hali ya kushangaza, baada ya kuona kamera wakaanza kufanyiana vituko vya kimahaba.

Shilole alionekana kumshikashika Medy huku dogo huyo aliyeonekana kuwa kama kalewa akitoa ushirikiano.Katika meza iliyokuwepo sebuleni kulikuwa na chupa za bia lakini mara kadhaa Shilole alionekana akinywa juisi huku dogo akipiga maji, mazingira yaliyoonekana kuwa Shilole alikuwa akimlewesha kwa makusudi kisha mambo ya ‘kuchi…kuchi’ yachukue nafasi.

SHILOLEQ2

Akizungumzia uhusiano wake na Medy, Shilole alikiri kuwa ndiye mpenzi wake kwa sasa na akawataka wanaodai anambemenda wakidhani ni mtoto wakae kimya.“Huyu ndiye laazizi wangu kwa sasa, ana kila sifa ya kuwa mume wangu na wala siyo mtoto, ni mtu mzima kabisa tofauti na Nuh,” alisema Shilole kisha kuendelea kumdekea jamaa huyo aliyeonekana kafa-kaoza kwa staa huyo.

Wakati Shilole akifanya yake, Nuh naye juzikati alitupia picha kadhaa mtandaoni akiwa kimahaba na demu mkali aliyefahamika kwa jina la Erah Erah anayedaiwa kuwa mpenzi wake.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364