-->

Chuchu Afunguka Kuhusu Weupe wa Mpenzi Wake Ray

Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mpenzi wa Ray Kigosi amefunguka na kusema hapendi watu wanapokuwa wana msema mchumba wake Ray Kigosi kuwa amejichubua na kudai anaamua kupuuza ila huwa hapendezwi na suala hilo.

CHUCHU233

 

Chuchu Hans alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ jana na kudai kuwa mpenzi wake huyo kwa sasa amependeza kutokana na maisha yake kubadilika kwani zamani kwake maisha yalikuwa magumu na muda mwingi alikuwa akitembea kwa miguu na kuhangaika kutoka kimuziki ndiyo maana alikuwa anaonekana vile.

“Unajua mimi huwa sipendi sana watu wanapozungumzia suala hilo ila kwa kuwa sisi ni watu maarufu inafika mahali unaamua kupotezea tu, unajua watu wanashindwa kuelewa kuwa maisha yamebadilika na saizi sanaa ina lipa ndiyo maana Ray Kigosi amebadilika na kutakata, unajua zamani maisha hakuwa na uwezo sana na alikuwa anahangaika na kutoka na muda mwingi alikuwa akitembea kwa miguu ndio maana alikuwa akionekana vile” Alisema Chuchu Hans.

RAY1

Kwa upande wake Ray Kigosi alikiri kuwa sasa amebadilika na kuwa mweupe na kusema siri kubwa ni yeye kunywa maji sana, kufanya scrub ndiyo maana amekuwa hivyo ila hajichubui kama ambavyo watu wanasema.

 

eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364