Shilole Alazwa Hospitali Baada ya Kuzidiwa Usiku wa Jana
Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Shilole amelazwa hospitali baada ya kuzidiwa usiku wa jana.
Akiongea na Bongo5, Babalevo ambaye yupo katika hospitali aliyolazwa muimbaji huyo iliyopo Kinondoni, amedai kuwa usiku wa jana alichemka kiasi cha kukosa nguvu na kulazimika kupelekwa hospitali.
Aliwekewa drip kushusha homa hiyo na madaktari wamemshauri apate muda wa kupumzika zaidi. Babalevo amesema Shilole ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akifanya mazoezi makali ya mwili anaendelea vizuri.
Tunakuombea upone haraka Shishi.
Chanzo:BONGO5