-->

Shilole Ampigisha Dj Tass ‘Sorry For That’ Mia Kidogo, Mitusi Live !

MWIGIZAJI na mwanamuziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemzingua Dj Tass mtangazaji wa kipindi cha Kwetu Fleva baada ya kushusha matusi hewani akihojiwa na mtangazaji huyo na kumfanya aombe msamaha kwa wasikilizaji kwa kutamka Sorry for That mara mia.

TASS

Tass alikatiza matangazo baada ya Shilole kuulizwa swali kuhusu mpenzi wake Shilole ambaye ametangaza kutengena naye hivi karibuni Mziwanda ambaye alitamba naye kwa muda mrefu na hata msanii huyu wa kiume kujichora picha ya Shilole mwilini mwake.

“Wapenzi wa kipindi cha Kwetu Fleva nawaomba radhi kwa kilichotokea Shilole waombe msamaha, na nimekukanya mara ngapi? Nitakuzingua upo hewani unatukana una maananisha nini? Sorry for that, sorry for that,”anasema Dj Tass.

Baada ya kuagana na Shilole wapenzi wa kipindi hicho wamelaumu Dj Tass kwa kumleta Shilole akiwa kalewa studio na kuharibu interview , msanii huyu alikuwa akimponda sana Nuhu Mziwanda akimtangaza msanii kutoka Uganda E Kenzo kama mchumba wake mpya kwa sasa.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364