Rose Ndauka: Wanaume Wakware Bado Wananisumbua
STAA wa filamu nchini, Rose Ndauka, ameweka wazi kwamba licha ya kujibidisha kwenye ubunifu wa kazi mbalimbali za kumwingizia kipato anazozifanya, hujikuta akikutana na idadi kubwa ya wanaume wakware wanaomtaka kimapenzi badala ya kufanya naye biashara.
Ndauka ambaye kwa sasa anajishughulisha na ujasiriamali, alisema amekua akibuni njia mbalimbali za kumwingizia kipato ili aendane na hali halisi ya maisha kwa sasa lakini wanaume wakware humkwamisha kwa usumbufu juu yake.
“Kila kazi ina changamoto zake, sikatai wanaume lakini wengi wao huja kunitaka kimapenzi, badala ya kuzungumzia masuala mengine ya biashara, nachukizwa sana na wanaume wa aina hii,” alieleza Ndauka.
Mtanzania