-->

Shilole Atoboa Siri ya Kupenda Vijana Wadogo

Mwanamuziki wa Bongo flava ambaye ana vimbwanga kila siku kwenye mitandao ya kijamii kwa skendo ya kutoka na vijana walio chini ya umri wake amefunguka na kusema asipangiwe ni nani wa kuwa naye.

Shilole-4

Akiongea mbele ya Camera za eNewz, Shilole amesema mashabiki wanahitaji yeye awe na mzee lakini yeye haoni haja ya kuwa na mzee kwa kuwa hawawezi ‘kumpetipeti’ na kuwataka wamuache achague anachotaka kwa vile nyumbani yeye ni Zuwena na jukwaani ni Shilole.

“This is my life, nikiwa nyumbani ni Zuwena na nikiwa kwenye TV ni Shihi, maisha yangu mimi ya nyumbani au maisha yangu binafsi wao yasiwahusu sana ninaangalia upendo wangu upo wapi. Nikisema niangalia mashabiki nini wanacho taka wao wanataka niwe na mzee, sasa maisha yangu nianze kuwa na mzee nianze kumburuza! mimi ninahitaji kijana aanze kunipetipeti” Alifunguka Shilole kwa madaha.

Lakini Shilole alimalizia kwa kusema kuwa mpenzi wake mpya wa sasa ni msanii wa muziki na wala hajawahi kubahatika kuwa na mpenzi ambaye ni dakitari au mwalimu, bali ana nyota ya kukutana na wasanii tu.

eNewz ilitaka kupenyeza zaidi kutaka kujua kisa cha msanii mkubwa kama yeye kuonekana kama video queen kwenye video tatu hadi sasa ikiwa ni pamoja na video ya Manfongo ‘Hainaga ushemeji’, Darasa ‘Too Much’ na Rayvan ‘Natafuta kiki’. Shilole aliweka wazi kuwa kuonekana kwenye video zote hizo ametokea kwa kuwa ana urafiki na wasanii hao akaona asiweke u’star’ kwakuwa hata yeye alisha wahi kuwa video vixen.

Akifafanua zaidi kwenye muonekano wake katika video ya Rayvan, Shilole amesema hakuvaa chochote ndani zaidi ya ‘night dress’, hivyo ilimbidi atupie kileo ili aweze kufanya scene hiyo.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364