-->

Filamu ya Naomba Niseme Yachaguliwa Tuzo Kubwa Africa

FILAMU bora kabisa ya Naomba Niseme iliyotayarishwa na Staford Kihore imeendelea kufanya vizuri katika tuzo mbalimbali na matamasha baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine katika tuzo kubwa Afrika za African Magic Viewers Choice Awards 2017, sinema hii fupi inapambana na filamu za watayarishaji wengine wakubwa.

Mzee Isaya mshiriki wa filamu ya Naomba Niseme

Historia inaonyesha kuwa filamu nyingi ambazo zimekuwa zikipenyeza katika matamasha kama haya ni zile zinazopata ruzuku kutoka katika taasisi kutoka nje lakini sinema ya Naomba Niseme ni kazi ya kijana mzalendo mpiganaji wa tasnia ya filamu ambaye ameweza kufanya kazi hiyo nguvu na kuingia katika ushindani.

Filamu Naomba Niseme ni sinema fupi iliyobeba ujumbe kuhusu Urithi kwa wanawake wajane bila ridhaa yao huku wakikosa kabisa nafasi ya kujieleza kwa wazee wa Mila na kusababisha matatizo huku jamii ikiteketea kwa maradhi mbalimbali kama Ukimwi na mengine.

Staford Kihore mtayarishaji wa filamu ya Naomba Niseme.

“Kuchaguliwa na ugombee katika tuzo kubwa kama hizi ni heshima kubwa sana kwani ni sehemu ya kukutana na watayarishaji wakubwa ambao pengine isingekuwa rahisi kukutana nao kwa ahadi tu,”alisema Kihore.

Sinema hiyo ya Naomba Nisema ni utunzi wa Myovela Mfwaisa na muswada umeandikwa na Myovela, katika vipengele viwili filamu hiyo inakutana na sinema nyingine ya Aisha iliyotayarishwa na Amli Shivji, Home coming ya Seko Seko na kufanya nafasi hiyo kutawala na watazania.

Naomba Nisema, Aisha zimeingia katika vipengele viwili Best Overrall Movie na kipengele cha Best Movie East Africa ambapo katika kipengele hiki inakutana na kazi nyingine ya Homecoming kutoka Tanzania pia ni fursa nyingine ya kuwabwaga Wakenya na wanaAfrika Mashariki.

Ni nafasi nyingine kwa Tanzania kuibuka kidedea kama tuzo zilizopita wakati filamu za Kitendawili na Mapenzi ya Mungu zilizoibuka na ushindi na kuwapatia tuzo Richie na Lulu kutoka Swahilihood.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364