-->

Sijamvisha Mtu Pete- Harmonize

Msanii kutoka katika label WCB Wasafi Harmonize ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya wa ‘Bado’ amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya hajawahi kuvalishwa pete ya uchumba na wala yeye hajawahi kumvalisha mtu pete ya uchumba na kudai mpenzi wake mpya Jackline Wolper amemkuta akiwa hana mtu na ndiyo maana wakaweza kuanzisha mahusiano.

Harmonizer na Wolper

Harmonize amesema hayo kupitia kipindi cha Enews ambapo alikuwa anaelezea mambo mbalimbali kuhusu maisha yake mapya katika mahusiano na Wolper ambaye yeye mwenyewe amekiri kuwa ni mtu aliyeanzisha naye mahusiano hivi karibuni na kusema tuwe na subira kila kitu kitakuja kuwekwa wazi siku za usoni.

“Unajua mpaka saizi sijamvisha mtu pete ya uchumba wala mimi sijawahi kuvishwa pete ya uchumba ila niseme tu ni kweli nipo kwenye mahusiano na Wolper ambaye ni maarufu kama mimi na wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi” alisema Harmonize

eatv.tv

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364