Sijui Kitu Gani Kinatusibu- Lulu
MWIGIZAJI wa Filamu na mshindi wa tuzo za African Magic Viewers Choice Awards (AMVCA) Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kwa kusema kuwa haelewi kitu gani kinawala wasanii wa filamu kukosa umoja na ushirikiano kwa kila jambo zaidi ya kuombena mabaya tu.
“Nimejifunza mengi sana katika tuzo za African Magic hasa kwa wenzetu wa Naijeria wanapendana sana kwani ilikuwa kila kipengele kikitajwa washindani wanapiga makofi, na akishinda mmojawapo wote wanamshangilia na kumpongeza,”anasema Lulu.
Lakini kwa upande wa Bongo hali ni tofauti mtu anapofanya vizuri katika tasnia ya filamu ndio kwanza anajikuta akitengwa na kusemwa vibaya badala ya kujiuliza kuwa kafanya nini ili wamwige na kutengeneza ushindani wa kweli kikazi, anasema hiyo ni changamoto kubwa kufika kimataifa.
FC