-->

Wasanii Wengi Bongo Wanatumia Unga – Babu Tale

Meneja wa wasanii wa muziki kutoka Tip Top connection Hamisi Tale Tale maarufu kwa Babu Tale, amesema kuwa wasanii wengi kwa sasa wanatumia madawa ya kulevya, na hii ni kutokana na kuiga mambo ya Marekani.

Babu Tale akiwa na Chid Benz

Babu Tale akiwa na Chid Benz

Babu Tale ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye Planet Bongo inayorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa alipokuwa akimpeleka rehab msanii Chid Benz, alimwambia kuwa wasanii wengi wanatumia unga (madawa ya kulevya) na kumtaka kuweka wazi ili jamii ijue, lakini aligoma kumtajia ni kina nani.

“Kikubwa alichokuwa anasema bosi unanisaidia mimi lakini wanatakiwa watu wajue watu kibao ambao wapo kwenye industry wanakula unga, wapo wasanii wa bongo movie wanakula unga, wapo bongo fleva wanakula unga”, alisema Babu Tale akiwa anamnukuu Chidi Benzi baada ya kumfikisha rehab.

Babu Tale amesema kwa sasa mpango wake mkubwa ni kumsaidia Chid Benz, na kusema kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na kuwa mzazi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364