Sikutoa ‘Muziki’ Kumfunika Mtu – Darassa
Nyota wa hip hop katika anga la bongo Fleva, Darassa amesema hakutoa ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Muziki’ kwa lengo la kufunika ngoma ya mtu mwingine bali ni kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii na kuwaburudisha mashabiki wake.
Darassa amefunguka hilo katika kipindi cha FNL cha EATV alipotakiwa kufafanua iwapo ni kweli kwamba alitoa ngoma hiyo ili kufunika ngoma ya msanii mingine mkubwa wa bongo fleva iliyotoka kipindi hichohicho.
“Sijatoa Muziki ili kufunika ngoma ya mtu yoyote, nimetoa Muziki kama sehemu ya mipango yangu” – Amesema Darassa.
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakizilinganisha baadhi nyimbo mpya zilizotoka hivi karibuni ambapo wimbo wa Darassa umekuwa ukilinganishwa na ngoma ya Kokoro iliyotolewa na Rich Mavoko akimshirikisha Diamond ambapo wengi wamekuwa wakidai kuwa ngoma ya Muziki ya Darassa imeifunika ngoma hiyo ya Kokoro.
eatv.tv