-->

Singeli Tuipe Nguvu Zaidi- Juma Nature

Msanii mkongwe wa bongo fleva Juma Kassim Nature amefunguka na kusema kuwa katika muziki Bongo ambao unaweza kupewa nafasi kubwa zaidi ni muziki wa singeli kwanza anasema ni muziki wenye asili yetu lakini pia ni muziki ambao tayari watu wanauelewa

Juma Nature alisema haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema vyombo vya habari pamoja na watanzania wanatakiwa kuupenda na kuwapa nguvu wasanii wa singeli ili muziki ule uweze kufika mbali na kuwa utambulisho wetu.

juma nature67

“Saizi kwa muziki ambao unatakiwa kupewa nguvu ni singeli, lakini kuna kitu kimoja bado kinanikera kwa baadhi ya wasanii wa singeli, maneno wanayotumia kwenye kutunga nyimbo zao inabidi wapunguze, wanatumia maneno makali sana ambayo si mazuri katika jamii zetu zinazotuzunguka, maneno yao mengi yanaamasisha mambo mabaya kwenye jamii” alisema Juma Nature.

Nature alizidi kusisitiza na kuwashauri wasanii wa Bongo fleva pamoja na singeli kuwa waangalifu kwenye utunzi kwa kuepuka kutumia maneno mabaya ambayo yanaleta athari kwa mashabiki mtaani na jamii kiujumla.

“Unajua hawa wasanii hawajui ni kiasi gani watu wanasikiliza nyimbo zao na kufanya mambo ambayo wao wanaimba, mtaani watu wanapata shida, watu wanakabwa, wanawake wanaporwa, yaani shida tupu mimi mwenyewe nimeshuhudia polisi wanapata taabu na watu, lakini ukiangalia matukio haya yanatokana na hamasa walizosikia kwenye nyimbo za wasanii, hivyo si vizuri tuandike vizuri tupunguze ukali wa maneno” alisema Juma Nature.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364