-->

Sipo kwa Ajili ya Kujiuza- Wastara

Staa wa Bongo Movie, Wastara Juma  ambaye siku za karibuni aliomba talaka kutoka kwa mume wake amefunguka na kusema yeye sio mtu wa kujiuza, bali ni mtu ambaye anajijali na kujitunza.

Wastara

Wastara

Wastara alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWS ambapo inasemekana kwa sasa kuna wanaume kibao ambao wanajitokeza kumtaka baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma.

Msanii huyo amesema kuwa ni kweli wapo wanaume wengi wanaojitokeza kumtaka na wengine wakija na ahadi ya ndoa lakini bahati mbaya wanaume hao wanakuja wakati yeye haitaji kuwa na mtu kutokana na jinsi alivyoumizwa.

“Mimi si mali ya mtu na wala sipo kwa ajili ya kujiuza, lakini ukweli ni kwamba wapo wanaume wa aina nyingi ambao wanakuja na kunitaka wengine wanakuja wakitaka ndoa kabisa na wengine unakuta kweli wanania ya dhati kabisa lakini wanakuja wakati mimi sijisikii kuwa na mwanaume, maana kitu kwa kitendo alichonifanya Sadif hakijaniweka sehemu nzuri” alisema Wastara.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364