Siri 5 za Ndoa ya Wastara Kuvunjika!
Saa 24 tu tangu kupatikana kwa habari kwamba, ndoa ya staa wa sinema za Bongo, Wastara Juma aliyoifunga na Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma imevunjika, sasa siri 5 za kuparaganyika kwa ndoa hiyo ziko mikononi mwa gazeti hili.
Ndoa hiyo ilidaiwa kuvunjika rasmi Machi 21, mwaka huu baada ya kuishi kwa siku 61 tangu kufungwa kwake, Januari 8, mwaka huu huko Tabata jijini Dar.
SIRI YA KWANZA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kimoja, miongoni mwa siri hizo zilizoisukuma ndoa hiyo kuvunjika ni kitendo cha Wastara kuomba kila kukicha kwamba, aachike baada ya madai kwamba, hakukuta furaha kama alivyotegemea.
“Wastara alitegemea kwamba baada ya kuolewa angekuta furaha. Lakini anavyosema jambo hilo silo alilokumbana nalo ndani ya ndoa. Hiyo ni siri moja wapo, ikamfanya Wastara amuombe Mungu kila siku ili aachike,” kilisema chanzo hicho.
SIRI YA PILI
Chanzo kiliendelea kudai kuwa, pia Wastara aliingia kwenye ndoa hiyo huku moyo wake wote ukibaki kwa mchumba wake wa zamani, Bond Suleiman.
“Wastara tangu akiwa ndani ya maamuzi ya akubali au akatae kufunga ndoa na Sadifa, alikuwa akisema moyo wake umeelekea sana kwa Bond.
“Hivyo naamini kuwa, hata alipoambiwa anapewa talaka aliipokea kwa mikono miwili ili arudi kwa Bond. Mimi naamini hivyo,” kilisema chanzo.
WASTARA MWENYEWE NA SIRI NYINGINE
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wastara alikiri kuvunjika kwa ndoa yake huku akisema:
“Tangu nifunge ndoa sijawahi kuwa na furaha ndani ya ndoa hata mara moja kwani mume wangu alikuwa akinifanyia mambo siyo.
SIRI YA TATU
“Kabla hajanioa, aliniahidi vitu vingi ikiwemo kunifungulia maduka kwa ajili ya kujiendeleza na vitu vingine vingi lakini hakuna hata kimoja alichokifanya,” alisema Wastara.
SIRI YA NNE
Staa huyo alikwenda mbele zaidi na kuanika siri ya nne akisema: “Nilipoona ndoa imenichosha nikawa najaribu kutishia kuondoka, nikimwambia naondoka alikuwa akiniambia njia nyeupe niondoke mapema ili mke wake (mkubwa) aje kuishi. Inaonekana alitamani niondoke ili mke wake aje kukaa nyumbani. Alisema mke wake hawezi kukaa hotelini na mimi nipo ndani.”
SIRI YA TANO
Ilidaiwa kuwa, siri nyingine iliyomfanya Wastara aachike ni kushindwa kwake kukabiliana na uke wenza hasa ikielezwa kuwa, uvumilivu wa hali ya juu unahitajika unapoingia kwenye ndoa ya sampuli hiyo.
“Unajua siri nyingine ni kwamba, Wastara siyo mwanamke wa kuvumilia uke wenzake, yapo baadhi ya mambo angevumilia lakini hakuwa mvumilivu, ikawa sababu ya yeye kuondoka,” alisema rafiki wa karibu wa staa huyo.
AONDOKA NA MSICHANA WA KAZI
Wastara alisema kuwa, ameamua kuondoka kwa mwanaume huyo yeye na msichana wake wa kazi ‘hausigeli’ kwa kuwa alishachoka.
ANACHOJUA WASTARA
“Mimi najua watu wengi watasema na kuniona tofauti lakini kikubwa naangalia furaha yangu iko sehemu gani, najuta sana kuingia kwenye ndoa lakini nawashauri wanawake wenzangu kufikiria mara mbilimbili kabla kuingia huko, kuna mambo mengi sana,” alisema Wastara.
HUYU HAPA MUME WA WASTARA
Sadifa Juma ndiye anayelalamikiwa na Wastara kwamba hakumtimizia yale aliyomwambia lakini pia ndiye anayedaiwa kumpa talaka Wastara na si kwamba, ameomba yeye.
Akijibu madai ya Wastara alipoongea na gazeti hili juzi kwa njia ya simu, alisema:
“Mimi si mgonjwa wa akili, Wastara ni mlemavu, hana baba wala mama halafu leo hii nimseme vibaya. Mpaka nimeamua kumuoa ina maana nilimpenda kwa nini nimfanyie vitu ambavyo sivyo?
“Lakini katika hayo, pia mimi nimefundwa kwa kufundishwa kwamba mambo ya ndoa hayapelekwi kwenye vyombo vya habari au Instagram. Na huyo aliyevianika vitu vya mke wangu nitadili naye.”
MSISITIZO WAKE
“Ninachojua mimi, Wastara bado ni mke wangu. Huyo mnayesema kwamba babu yake ameongea kwenye redio akisema kwamba nimemwacha Wastara, talaka alitoa yeye? Mambo ambayo mimi naweza kuyasema kwenye vyombo vya habari ni kuhusu jimbo langu au mambo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni chama changu.”
BOND: MIMI NIMESIKIASIKIA TU
Ijumaa lilimpigia simu Bond juzi na kumuuliza kuhusu Wastara kuachika ambapo alisema: “Na mimi nimesikiasikia na kusoma kwenye mitandao, hivi ni kweli?” (Ijumaa likaachana naye bila kumpa jibu).
MAISHA YA UHUSIANO, NDOA YA WASTARA
Wastara amapitia katika maisha ya uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa. Mwaka 2000 alifunga ndoa na mwanaume anayeitwa Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares.
Nyuma ya hapo, Wastara alizaa mtoto mmoja na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.
Mwaka 2003, Wastara alifunga ndoa na msanii mwenzake wa filamu, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye alifariki dunia mwaka, 2013. Walibahatika kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Farheen.
Mwaka 2015, akafunga ndoa na Mbunge Sadifa akitokea kwenye uhusiano na msanii wa filamu, Bond na aliyodai kuyasema ndiyo hayo kwamba ameachika kwa talaka mbili huku mumewe huyo akikanusha.
Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni, habari zilitua Ijumaa kwamba Wastara ameugua ghafla baada ya sukari kupanda akiwa mjini Morogoro na kulazwa Hospitali ya ST. Herry Health
Chanzo: GPL