-->

Filamu Kubwa ya Action ya ‘Omba’ Kutikisa Bongo!

Omba89

FILAMU ya Mapigano ijulikanayo kwa jina la Omba imekamilika na muda si mrefu itaingia sokoni ni kazi kutoka kwa mwanadada Christina Mroni ‘Tina’ ambaye ameigiza kama kinara wa filamu hiyo ambayo inakuja kuleta mabadiliko makubwa Swahilihood.

Jumbe

Frank (Jumbe) mwigizaji ambaye ameigiza kama Rais katika sinema ya Omba.

Omba film

Filamu ya actions ya Omba kutoka Swahilihood

Akiongea na FC mtayarishaji wa filamu hiyo Tina amesema kuwa kiu yake ni kuwa na kitu tofauti katika tasnia ya filamu hivyo alitumia muda mwingi sana katika maandalizi ya kazi ya kipekee ambayo ni filamu ya mapigano ya Omba sinema yenye mikiki mwazo mwisho.

“Ukitaka kitu kizuri kinahitaji muda na kujipanga zaidi siku zote nataka kufanya kitu tofauti na kinachokubalika katika jamii filamu ya Omba ni kazi nzuri iliyojaa upelelezi, maarifa na ujuzi wa hali ya juu, actions si kazi ya kuikosa,”anasema Tina.

Filamu ya Omba ni filamu ya kipekee kutengenezwa Bongo ikiwa chini ya mwanadada mahiri katika utengenezaji na uigizaji na imeshirikisha nyota wengi wenye ujuzi kwa maelezo na lini itakuwa dukani kila siku pitia mtandao huu tutakujuza.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364