Wema: Sijawahi ‘Kummisi’ Kajala, Muna
STAA wa filamu mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa hajawahi kuwakumbuka (kuwamis) waliokuwa mashoga zake wa damu, Muna Alphonse ‘Muna’ na Kajala Masanja na kudai alishawatoa kwenye akili yake.
Akizungumza na Star Mix, Wema alisema kuna baadhi ya watu ambao hajaonana nao muda mrefu na anawakumbuka kila mara lakini kwa upande wake hajawahi kuwakumbuka rafiki zake hao ambao huko nyuma walikuwa kama kumbikumbi.
“Sitaki kusema dhambi jamani sijawahi kuwamisi hawa watu (Muna na Kajala) kabisa naona kama niliwafuta kwenye kichwa changu maana najikuta kuna watu nawakumbuka lakini hao hapana,” alisema Wema.
Chanzo:GPL