-->

Siwema Amuumbua Nay wa Mitego

SIKU chache baada ya mzazi mwenzake na msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego,’ Siwema Edison kutoka gerezani na kutakiwa atumikie kifungo cha nje, amefunguka ya moyoni huku akimuumbua ‘zilipendwa’ wake huyo aliyekuwa akidai alipambana kumsaidia.

nay12

Siwema na Nay wa Mitego

Chanzo makini cha habari hii kilitutonya hivi karibuni kuwa, mbwembwe zote alizokuwa akizitoa Nay kuwa yeye ndiye kila kitu mpaka Siwema akarejea uraiani, si za kweli na zimemuumiza msichana huyo, kwani hakufanya chochote kumsaidia kwenye janga hilo.

“Siwema analalamika sana, anaumizwa na majigambo ya Nay kuwa jitihada zake ndiyo zimemrejesha uraiani kitu ambacho si cha kweli. Ndugu wa Siwema walikuwa ndiyo kila kitu kufanikisha mtoto wao anaondoka kwenye majanga hayo, sasa hata haieleweki kwa nini Nay ameamua kuongea uongo kiasi hicho kwenye ‘midia’,” kilifu-nguka chanzo hicho.

Baada ya gazeti hili kunasa ‘ubuyu’ huo, lilimtafuta Siwema aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia ya vitisho kutoka kwa kigogo mmoja, alipopatikana alifunguka kama ifuatavyo:

“Dah! Kweli hivi vitu vinaniumiza sana. In short (kwa kifupi) sitaki kumzungumzia sana Nay maana ni mzazi mwenzangu tayari ila nashangaa anavyozungumza kuwa amenisaidia wakati si kweli.

“Kiukweli walionisaidia na kunipigania ni ndugu zangu na mpaka leo nipo hapa. Ninachokumbuka kuhusu Nay najua alikutanaga na rafiki yangu, akampa laki tatu kwa ajili ya kunisaidia nikiwa gerezani, basi.”

Msikie Nay

Alipotafutwa Nay kuzungumzia habari hiyo alisema: “Kwa namna moja ama nyingine, sitaki kuzungumzia chochote, Mungu ndiye anayejua ukweli wote na kama wanasema mimi sikushiriki kumsaidia basi naomba radhi kwa hilo. Nisamehewe!”

Siwema yuko huru kabisa?

Risasi Mchanganyiko lilichimba zaidi kuhusiana na kutoka gerezani kwa Siwema ambapo ilibainika kuwa, yuko kifungo cha nje huku akifanya shughuli za kijamii kwenye kituo kimoja cha afya kilichopo Mwanza.

“Siyo kwamba nipo huru kabisa, hapana. Huku Mwanza kuna sehemu naweza kusema ni kituo cha afya huwa nahudhuria kwa ajili ya kuripoti na kutimiza masharti ya kutumikia kifungo cha nje, naweza kukwambia hivyo kwa sasa,” alisema Siwema.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364