Siyo Lazima Sote Tubanane Dar –Vinego
MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu Bongo Baraka Selemani ‘Vinego dizaina’ amewashauri watayarishaji wa filamu kutoka mikoani wasikimbilie wote Dar es salaam kwa sababu ndio kwenye soko la filamu bali wajikite mikoani kama anavyofanya yeye kwani huko ndio kuna mazingira mazuri .
“Mikoani kuna mazingira mazuri sana ya kutengenezea filamu kwani kuna uhalisia sana kuliko huku Dar, nimefanikiwa kurekodi filamu Singida na sasa nipo Chunya kuna mazingira safi sana huku maisha ya wachimba madini kulingana na hadithi yangu,”anasema Vinego.
Vinego anasema kufanyia sinema mkoani kunakuza vipaji kwani nchi ina wasanii wengi wenye uwezo lakini shida ni kwamba hawafikiwi na watayarishaji wengi ambao wakihama Dar watahamia Morogoro tu na si nje ya hapo msanii huyo anatamba na filamu yake mpya ya Aiyola.
FC